Feedback Sitemap Send page Print Help
SchoolNet inamaanisha nini

Ingawa jedwali hapa chini linaelezea mpangalio wa schoolnet, pia linatoa mwangaza juu ya maana halisi ya "school networking". Tunaona ni lazima kuwe na:

  • mawasiliano ya mara kwa mara na ushirikiano kati ya mashule
  • Mafunzo kwa walimu na wanafunzi katika matumizi ya teknolojia.
  • Miradi ya ushirikiano miongoni mwa shule mbalimbali. 
  • uendeshaji na ushirikiano wa mitaala na iliyomo kwenye elimu.

MUUNDO

HUDUMA

UENDELEZAJI

Uanzishaji na undelezaji wa taasisi/asasi za schoolnet

Kima cha chini kina shule 5 kwa mawasiliano ya kawaida na ushirikiano kwenye njia za kujifunza kwa kutumia habari,vyombo vya mawasiliano na teknolojia

 

Usambazaji na uunganishaji wa kompyuta unatolewa na taasisi ya schoolNet

Miradi ya ushirikiano miongoni mwa shule kwa kutumia mwongozo mpana wa teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT).

Uendelezaji na ushirikiano wa mitaala na yaliyomo kwenye elimu

Mafunzo kwa walimu kuhusu ICT ili kuboresha ufundishaji

Ukuzaji wa mwaka hadi mwaka wa schoolnet katika nchi husika

Uwezo wa kujitegemea kifedha kuongezeka mwaka hadi mwaka kukiwa na upungufu wa mategemeo kutoka nje.

Ongezeko la nguvu kazi mwaka hadi mwaka bila kutegemea nguvu kazi kutoka nje.

Uimarishaji wa ushirikiano mwaka hadi mwaka

Chanzo: http://www.schoolnetafrica.org

Hivyo basi, School networking sio tu inahusika na upatikanaji wa habari na mawasiliano ya kiteknolojia mashuleni, bali hata matumizi ya teknolojia hii kama njia ya kuhamasisha shule kufanya kazi pamoja ili kuboresha nafasi za shule katika bara la Afrika. Hii inahusisha matumizi ya ICT kwenye madarasa kwa malengo ya uongozi na utawala. Mitandao mashuleni inahusisha mambo zaidi ya utambulishaji wa kompyuta kwenye mashule (ingawa hili ni jambo muhimu), hii inamaanisha kwamba shule zinapata uwezo wa kufanya kazi pamoja na kushirikiana katika vyanzo, hivyo kuwa bora zaidi.

Kuanzisha SchoolNet ya kitaifa

Hatua ya kuanzishwa kwa schoolnet katika Afrika mara nyingi huanza nje ya muundo wa kiofisi wa asasi za serikali katika nchi husika. Kwa namna nyingi schoolnet huanzishwa na watu wanaojitolea wakifanya kazi katika asasi zisizo za kiserikali (NGO's) bila kuwepo kwa nguvu kutoka serikalini. Zifuatazo ni hatua muhimu za kuanzisha schoolnet katika mazingira ya Afrika.

1. Bingwa/mabingwa waliojitolea

Kunatakiwa kuwa na mtu wa kuendesha hatua za awali katika hali inayotazamiwa. Hatua kama hii imefanikiwa katika nchi mbali mbali. Kwa kawaida, ni mtu mmoja anayeamua kuchukua jukumu la kuanzisha hatua ya awali. Bingwa/Mabingwa waliojitolea watachukua majukumu ya hatua zilizobaki

2. Tambua ni nini hasa unataka na wapi unataka kuanzia

Ni muhimu kutambua shule ambazo unazilenga, jinsi ambavyo utatoa kompyuta kwenye shule hizo, jinsi ambavyo utawafunza walimu na jinsi ambavyo utaendeleza miradi ya ushirikiano.

Mara nyingi ni busara kuchagua miradi miwili au mitatu ambayo unaweza kuiendeleza na kuiinua ili kuanzisha schoolnet

Ni lazima ufahamu namna ya:

o Kuchagua shule;

o Kuchagua walimu watakaohusika;

o Kuchagua wanafunzi/ wajifunzaji watakaohusika

o Kuangalia vyanzo vitakavyohusisha mashule, waalimu na wanafunzi

Utahitaji kuwa na uwezo wa kuchagua na kueleza kila moja ya mambo yaliyo hapo juu ili kuhakikisha kwamba unahusika na sehemu mojawapo ya mfumo wa elimu.

3. Kupata washika dau

Baada ya kutambua mambo unayohitaji na namna ambavyo utayafanyia kazi, ni muhimu kuhamasisha washika dau na jumuiya mbali mbali ili kuweza kupata msaada katika mradi wenu

Jumuia za shule

Hili huenda likawa ni ndiyo kundi muhimu la washika dau ambao utaomba msaada wao. Hapa panahusisha; wakuu wa mashule/vyuo, walimu na wanafunzi kutoka katika shule unazozilenga watakuwa muhimu.

Serikali:

Kupata washika dau kutoka Wizara ya elimu, wizara ya mawasiliano, Wizara ya sayansi na teknolojia na wizara ya viwanda na biashara ni muhimu sana. Ni muhimu kujua mtu sahihi wa kuzungumza na wahusika wa wizara hizi.

Sekta huru

Kupata msaada kutuka kwa wasambazaji wa mtandao wa Intaneti kwenye nchi yako kwa kuwahamasisha kusambaza Intaneti kwenye mashule ni muhimu. Itakuwa pia muhimu kupata msaada kutoka katika mashirika yanayohusiana na habari na mawasiliano ya kiteknolojia katika ngazi za kitaifa na kimataifa, ambayo yanaweza kuwepo kwenye nchi yako. Kampuni za mawasiliano, kampuni za luninga, vituo vya redio…haya ndiyo makampuni ambayo misaada yao lazima iombwe. Pia kupata msaada kutoka kwenye sehemu zinazotoa huduma ya Intaneti imejaribiwa kwenye baadhi ya nchi.

 

Asasi za Jumuia na NGO's zingine:

Hizi ni baadhi ya asasi za washika dau ambazo zinahitaji kufikiriwa:

o Asasi za waalimu na vyama vya biashara

o Asasi za wanafunzi

o Bodi za wazazi

o Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO's) yanayojihusisha na ICTs  yanayofanya kazi katika nchi yako.

Asasi za kimataifa:

Kuna asasi mbali mbali ambazo unaweza kupata msaada kimataifa, mifano inajumuisha:

o ChildNet International;

o International Education and Resources Network (I-EARN);

o SchoolNet Africa;

o World Links Organization;

o Global Teenager Project of the International Institute for Communication and Development; and

o The Imfundo Project.

Tovuti ya schoolnet Africa ina habari zote kuhusu mashirika yaliyotajwa hapo

juu.

 

4. Kuitisha mkutano wa washika dau

Katika baadhi ya sehemu, kama Kenya washirika wetu waliitisha mkutano wa Washika dau kwenye nyanja hii ili kujadili baadhi ya mawazo ya kuanzisha

schoolnet. Kwa kutumia njia hii, utakuwa umefanya kazi ya msingi katika kupata msaada, kupata wadhamini na kufikiri kuhusu mawazo yatakayounda schoolnet

na kuikuza. Wakati mwingine kazi ya maandalizi inahusisha kudadisi asasi na makundi ambayo tayari yanafanya kazi kwenye ICT's mashuleni kwenye nchi

yako. Hii inaitwa "udadisi wa mazingira" Environmental Scan.

 

5. Kutengeneza biashara na miundo mbinu

Kuandaa mpango ambao utaongoza kazi kwa miaka mitatu ya mwanzo ni muhimu sana. Mpango huo lazima uhusishe mtizamo wa schoolnet na malengo ya schoolnet. Mtizamo mara nyingi uwe mbali ambao unaulenga na kufikia malengo ni njia ambayo schoolnet itafikia mtizamo wake.

Katika kuandaa mpango wa biashara, mafikirio lazima yalenge mambo yafuatayo

1. Ni miradi ipi ya awali ambayo itaanzisha asasi?

2. Jinsi gani utaanzisha miradi hii?

3. Jinsi gani utapata fedha za kuanzisha miradi hii?

4. Watu gani watakuwa washirika wakuu katika miradi hii?

5. Ni asasi ya aina gani utaanzisha?

6. Jinsi gani utahakikisha unamudu asasi, na kutokuwa tegemezi kifedha kutoka kwa wafadhili?

 

Hii ni baadhi ya mifano ya biashara za kawaida:

Hii ni baadhi ya mifano ya biashara za kawaida:

Vitu muhimu vya kujua kwenye kuandaa mpango wa biashara wa Schoolnet

  • Mpango wa biashara ni muhimu.
  • Isiwe imenakiliwa.
  • Ni nyaraka muhimu ambayo unaweza kuiangalia muda baada ya muda.
  • Itajaribu kuelezea kwa usahihi mambo ambayo utakuwa unayafanya katika miaka mitatu ya mwanzo na mambo ambayo mtakuwa mmeyafikia baada ya miaka mitatu.

Uchaguzi wa taasisi kwa uanzishwaji wa schoolnet

Wakati wa kuanzisha schoolnet, kuna uchaguzi wa taasisi zifuatazo, ambazo unaweza kufuata:

1. Anzisha mradi kwenye chuo kikuu au taasisi changa kama miradi shiriki;

2. Anzisha NGO inayojitegemea

3. Anzisha kama mradi shirika wa wizara ya elimu (kama una wadhamini wa kutosha kutoka wizarani).

4. Anzisha kama mradi usiolenga faida kwenye wasambazaji wa Intaneti (ISP) au biashara ndogo.

Angalia mifano na Ujuzi uliotumika katika kutengeneza Telecenters, Unaweza kutumia huu kama mwongozo katika kuanzisha SchoolNet